Wabunge waliidhinisha mashambulizi dhidi ya IS Jumatano na muda mfupi baadaye ndege za jeshi la anga la nchini hiyo zikaangusha mabomu kwenye ngome za kundi la IS.
Ripoti zinasema ndege hizo kwa mara nyingine zimeshambulia visima vya mafuta, na kwamba ndege mbili aina ya Tornado zilifanya shambulio kwa mara ya kwanza na kulipua visima saba vya mafuta wakati leo ndege mbili aina ya Typhoon na Tornado mbili zimefanya shambulio kwenye ngome ya IS.
Mapema Alhamisi, ndege nne aina ya Tornado ziliangusha mabomu katika visima vya mafuta vya Omar vilivyopo Mashariki mwa Syria.
Ndege hizo zinatumia kambi ya RAF iliyoko Akrotiri nchini Cyprus na hakuna vifo wala majeruhi walioripotiwa kutokana na shambulio hilo.
Ijumaa, Bunge la Ujerumani nalo liliidhinisha kutolewa kwa usaidizi wa kijeshi kwa vikosi vinavyopambana na wapiganaji hao nchini Syria.
Juhudi za mataifa ya Magharibi dhidi ya kundi hilo zimezidishwa tangu kuuawa kwa watu 127 kwenye mashambulio kadhaa mjini Paris, Ufaransa mwezi uliopita.
Note: Only a member of this blog may post a comment.