Tuesday, September 13, 2016

Unknown

Nuh Mziwanda Afunguka Jinsi Dully Sykes Alivyoikwamisha Mipango Yake

Msanii wa Bongo Fleva Nuh Mziwanda ametuambia kuwa ameshindwa kuendelea na mipango yake ya kuiachia ngoma yake ambayo alikuwa kaipa jina la “Inde” kutokana na Dully Sykes ameachia ngoma yenye jina kama hilo hivi karibuni. 

Mziwanda amedai kuwa ngoma hiyo aliifanya kitambo na ilipikwa na Producer Allo Name wa Zanzibar, na inasemekana kuwa Producer huyo ana uhusiano wa karibu sana na Prince Dully Sykes kiasi kwamba hadi katika computer ya kazi za Producer huyo ameweka wallpaper ya picha za Dully Sykes. Ikiwa ndio kitu ambacho kina muumiza sana kichwa Nuh Mziwanda na kuhisi kama kuna chochote kimetendeka baina ya wawili hao.

Kibongo bongo kuna ngoma kibao ambazo zimeshatoka huku zikiwa zina fanana majina. Na moja wapo ni “Mawazo” ambayo alianza kuitoa msanii Buibui mwezi May mwaka 2012 na baadae mwezi November mwaka 2013 mtu mzima Diamond Platnumz kuja kuachia yakwake ambayo nayo pia aliipa jina la “Mawazo”.
Lakini kwa Nuh mziwanda huo ameona sio mchongo kabisa na ameamua kutemana kabisa na ngoma hiyo na imembidi aanze mipango ya kuisuka ngoma nyingine kabisa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.