Thursday, September 15, 2016

Unknown

Mke wa Bilionea MENGI, Jacqueline Azindua Duka La Furniture za Nyumbani ‘Amorette’ [+Pichaz]

Miss Tanzania 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi, Alhamisi hii amezindua duka lake jipya ‘Amorette’ lililopo Sea Cliff Masaki jijini Dar es salaam ambalo litakuwa likiuza furniture za ndani za brand yake ya ‘Molocaho’.

Jacqueline Mengi akiongea na waandishi wa habari
Duka hilo kunauza vitu vya aina tofauti tofauti kama makochi, viti, vitanda, meza na baadhi ya vitu vingine huku akitarajia kuongeza kwa kuuza furniture za jikoni kwa hapo baadae.

Akiongea katika uzinduzi huo Alhamisi hii, Jacqueline Mengi amesema kuwa mahitaji makubwa ya furniture za majumbani ni kitu ambacho kimemsukuma kufanya biashara hiyo.

“Amorette ni kampuni ambayo nilianzisha miaka michache iliyopita, tunafanya interior designing. Kwahiyo ndio nikaanzisha brand inaitwa Molocaho, kwa hiyo bidhaa zote ambazo zitakuwa zinazalisha hapa zitakuwa na nembo ya Molocaho,” alisema Jacqueline.

Aliongeza, “Nilianza kudisign furniture kwa sababu niliona kuna ukosefu wa furniture ambazo ni unique, kwahiyo nikaona kwamba hii ni nafasi nzuri ya mimi kutengeneza furniture ambazo zitakuwa ni tofauti na ambazo zinapatikana kwenye market, lakini pia kutengeneza vitu ambavyo vipo kwenye viwango vya kimataifa. Mimi kama designer kwangu najisikia furaha kutumia muda wangu kudisign vitu.”

Jacqueline Mengi akiwa na Balozi Juma Mwapachu pamoja na wageni wengine waalikwa

Jacqueline Mengi akiwa na rafiki zake











USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.