Monday, September 5, 2016

Unknown

DOGO JANJA Adai ‘Kidebe’ Inaendelea Kumshangaza Kila Kukicha

Dogo Janja ni mtu mwenye furaha – shukrani kwa kasi ya mradi wake mpya, Kidebe ambao video yake inazikimbiza views za YouTube kuliko kawaida.

Ametuambia kuwa kazi hiyo imepata mapokezi yanayoendelea kumshangaza.

“Hata Youtube views this time around zinaenda kwa speed, kila nikiingia naona wakiongezeka kwa kasi kubwa sana,” amesema. “Namshukuru mwenyezi Mungu ni jinsi gani inaonesha naendelea kupanda ngazi katika kazi yetu,” ameongeza.

Kuhusu gharama za video yake, Janjaro amedai kuwa si busara kutaja kiasi lakini anakiri kumgharimu mkwanja wa kutosha. Hadi sasa video hiyo iliyoongozwa na Hanscana ina views zaidi ya laki 3 YouTube.

 “Ni video ambayo haiongopi, kila kitu kipo open kabisa hata ukiangalia vitu ambavyo vimefanyika mule, ni mtu anaweza kujiongeza mwenyewe, lakini ni video ya gharama kubwa,” amesisitiza rapper huyo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.