Monday, September 5, 2016

Unknown

Watayarishaji wa ‘EMPIRE’ Watoa Sababu ya Kid Cudi Kujitoa Kwenye Series Hiyo

Rapper Kid Cudi kutoka Good Music amejitoa kwenye kuigiza show kubwa ya TV ‘Empire’ siku chache kabla ya msimu wa tatu kuanza kuoneshwa.
Watayarishaji wa show hii wanasema Kid amejiondoa baada ya kutofautiana na waandaji katika masuala ya ubunifu wa uhusika wake. Nafasi ya Kid Cudi imeshachukuliwa na mtoto wa Master P, Romeo Miller maarufu kama Lil Romeo.

Romeo atakuwa akijulikana kama Gram ambaye ni mpenzi mpya wa Tiana na pia atakuwa hasimu mkubwa wa rapa Hakeem.
Kid Cudi tayari alikuwa amesharekodi baadhi ya vipande vyake na ameshaonekana kwenye trailer ya show ya msimu wa tatu.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.