Monday, April 11, 2016

Anonymous

TYGA Ampa Tano Blac Chyna, Hofu Kwa Mwanaye!

Mwanamuziki wa Marekani, Tyga.
WAKATI Blac Chyna akijiandaa kubadili jina na kujiita Angela Kardashian kufuatia kuchumbiwa na mpenzi wake, Rob Kardashian, aliyekuwa mpenzi wa modo huyo, Tyga amesema wala hajali kuhusu tukio hilo zaidi anamuwazia mwanaye, King Cairo.

Hivi karibuni Blac Chyna alivishwa pete ya uchumba na Rob ambaye ni kaka wa familia ya Kardashians yenye thamani ya dola 325,000. Wakati Tyga ni mzazi mwenzake na Blac ambaye alizaa naye wakati wapo kwenye uhusiano kabla ya kuvunjika na kuingia kwenye uhusiano na Kylie Jenner.

Juzikati, Tyga aliulizwa anajisikiaje baada ya mzazi mwenzake kuvishwa pete ya uchumba ambapo alifunguka kuwa kila mmoja anastahili kuwa na furaha hivyo haoni haja ya kuchukia zaidi ni kuona mama aliyemzalia mwanaye anakuwa na furaha huku akidai kikubwa kitakachompa wasiwasi ni maisha ya mwanaye.
“Ninajisikia furaha kwa kuwa mama wa mwanangu naye ana furaha lakini kitu kikubwa ambacho pengine nitajali ni maisha ya mwanangu. Nataka awe kwenye mazingira mazuri,” alisema Tyga

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.