Richard Bukos, Kilimanjaro
Wahenga walisema utakiona cha mtema kuni! Ndivyo ilivyomtokea kijana anayedaiwa ndiye sharobaro maarufu eneo la Himo katika Jimbo la Vunjo, Kilimanjaro aliyejitambulisha kwa jina la Steven Charles baada ya kumfanyia fujo mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli katika jimbo hilo wakati akinadi sera zake.
Katika tukio hilo lililoshuhudiwa na Ijumaa Wikienda lililokuwa eneo la tukio, Dk. Magufuli akiwa anaendelea kumwaga sera katika mkutano huo uliohudhuriwa na umati mkubwa, Steven alidaiwa kuanzisha fujo katikati ya umati huo na kusababisha mkutano kutawaliwa na vurugu huku watu wakishindwa kumsikiliza mgombea huyo.
Vurugu hizo zilipoongezeka, Dk. Magufuli alisimamisha zoezi la kunadi
sera zake na kuwaomba wanausalama kumdhibiti kijana huyo aliyekuwa
akifanya vurugu wakati akizungumza na wakazi wa eneo hilo.

Kijana huyo akiwa mikononi mwa dira.
Wahenga walisema utakiona cha mtema kuni! Ndivyo ilivyomtokea kijana anayedaiwa ndiye sharobaro maarufu eneo la Himo katika Jimbo la Vunjo, Kilimanjaro aliyejitambulisha kwa jina la Steven Charles baada ya kumfanyia fujo mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli katika jimbo hilo wakati akinadi sera zake.
Katika tukio hilo lililoshuhudiwa na Ijumaa Wikienda lililokuwa eneo la tukio, Dk. Magufuli akiwa anaendelea kumwaga sera katika mkutano huo uliohudhuriwa na umati mkubwa, Steven alidaiwa kuanzisha fujo katikati ya umati huo na kusababisha mkutano kutawaliwa na vurugu huku watu wakishindwa kumsikiliza mgombea huyo.
Kijana huyo akiwa mikononi mwa dira.
Baada ya kusikia amri hiyo, kundi la maafande wa FFU almaarufu Fanya
Fujo Uone lilikwenda kumchomoa Steven sehemu aliyokuwa akihamasisha
vurugu na kumbeba msobemsobe huku wamemkwida shati na kwenda kumtia
kwenye karandinga.
Shuruba alizozipata kijana huyo ndani ya dakika kama nne zilitosha
kabisa kulinganisha kibano hicho na kilichomtoa khanga manyoya kama
isemavyo kauli ya wahenga.
Note: Only a member of this blog may post a comment.