Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson.
Dar es Salaam: Mnyoosho! Kaulimbiu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli
‘JPM’ ya kutumbua majipu na watu wasiolipa kodi imemdondokea staa wa
sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson baada ya gari lake aina ya Audi
kukamatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa tuhuma za kuingizwa
nchini kinyemela bila kulipiwa ushuru na kukwepa kodi.
Habari kutoka kwa vyanzo vya kuaminika zilieleza kuwa tukio la Aunt
kutumbuliwa lilijiri hivi karibuni ambapo staa huyo alikuwa akificha
siri hiyo isinaswe na mapaparazi wetu, jambo ambalo limemshinda.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Wikienda lilimsaka Aunt kutaka kujua
kisa kamili ambapo alipobanwa alikiri kukamatwa kwa gari lake hilo kwa
makosa ya kukwepa kodi wakati linaingizwa Bongo hivyo kuwa mikononi mwa
TRA.
“Kweli gari langu limeshikiliwa na TRA ila haina tatizo sana kwani
wamekagua, karibia kila kitu kipo sawa isipokuwa ninadaiwa kodi tu
ambayo nayo si fedha nyingi kiasi cha kunishinda. Waliniambia vibali
vyake vyote viko sawa na kwamba lipo nchini kihalali kabisa hivyo
ninachotakiwa kulipia ni kodi tu ambayo najipanga kulipia muda wowote.
“Natafuta Sh. milioni 10 na kitu ili niweze kulikomboa,” alisema Aunt
aliyedai gari hilo alinunuliwa na baba mtoto wake, Moses Iyobo ‘Moze’
huku akigoma kutaja bei yake.

Note: Only a member of this blog may post a comment.