Picha za Davido na Wizkid wakiwa pamoja
sio picha zinazotokea au kupigwa kila siku, kumbuka wawili kuwa na beef
ambapo mwaka mmoja uliopita Davido alinukuliwa akisema ‘Wizkid
hanipendi… toka nimeanza kujulikana kimuziki nimekua nalinganishwa au
kupambanishwa na Wizkid, kitu watu hawajui sikuwahi kuwa na tatizo nae
na tulikua tunakutana backstage na night club na tulikua poa tu‘
Wizkid aliwahi kuhojiwa na mtangazaji huyuhuyu pia akasema Davido
anamuonea wivu sababu ya mafaniko yake…. haya yooote yalipita na wawili
hawa wakaja kupatana na sasa wako poa na hata waliahidi kutoa single
pamoja.

Kwenye Interview ambayo Davido akiongelea kutokupatana kwake na Wizkid
Kwenye Interview ambayo Davido akiongelea kutokupatana kwake na Wizkid
Tukiachana na hayo ya beef kitambo,
mpya ni hii baada ya Davido kufanya bonge la show weekend iliyopita huko
Congo Brazaville kilichochukua headlines April 4 2016 ni picha ya pamoja ya Wizkid na Davido ambayo ilipostiwa na Davido wakiwa kwenye ndege binafsi na aliandika ‘nimerejea Lagos na kaka yangu Wizkid’
Post ya picha ya Wizkid na Davido kwenye Twitter imekuwa
RETWEETED na watu wengi ambao ni zaidi ya 800 mpaka mara ya mwisho
naitazama tofauti na post zake nyingine zilizotangulia.
Wizkid naye alipost picha hiyohiyo kwenye page yake ya Instagram na kuandika ‘kileleni… sisi pekee’ ambapo
mashabiki wengi wameonekana kufurahishwa na watu hawa ambao walionekana
kuwa na uhasama, mashabiki wengine wamelilia ifanyike kolabo yao.

Note: Only a member of this blog may post a comment.