Friday, April 1, 2016

Anonymous

NUH Ammwaga Mrithi wa SHILOLE KIUNO

 
mziwanda
Mkali wa Bongo Fleva, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.
Stori: mayasa mariwata
MKALI wa Bongo Fleva, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amefunguka kuwa, amemmwaga mpenzi wake aitwaye Erah Erah licha ya kwamba penzi lao lilitawaliwa na mbwembwe nyingi.
Akipiga stori na paparazi wetu kuhusiana na maendeleo ya penzi lao, Nuh alifunguka kuwa demu huyo haikuwa riziki kwake kwani hakudumu naye baada ya kugundua hamfai na penzi lao limedumu kwa wiki mbili tu.
demu mpya wa nuhu 
Nuhu akiwa na aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wake, Erah Erah.
“Yule nimeshatemana naye, nitampata mkali zaidi yake,” alisema Nuh na kuongeza:
“Nilikuwa na Shilole, nikamuacha, nikampata Erah ambaye naye nimemuacha, naamini nitampata mkali zaidi yao.”
Nuh na Shilole walimwagana hivi karibuni huku kila mmoja akidai hakuwa na amani kwenye uhusiano huo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.