Stori: Mayasa Mariwata na Hamida Hassan, Ijumaa
Dar es Salaam: Baada ya hivi karibuni kukiri kanisani kuwa ameokoka na kumkubali Mungu kuwa bwana na mwokozi wake kisha kukengeuka na kupiga picha chafu za nusu utupu, waumini wamemlipua staa wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ (pichani akiwa na biblia) kwa madai kuwa anatia aibu.

TUJIUNGE KANISA LA MAKUTI-KAWE
Mara baada ya kushinda Tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Filamu Afrika
Mashariki nchini Nigeria mapema mwaka huu kupitia Filamu ya Mapenzi ya
Mungu, Lulu alihudhuria ibada kwenye Kanisa la Living Water Centre
(Makuti-Kawe) la Apostle Onesmo Nyakura Ndegi lililopo maeneo ya
Mahakama ya Zamani, Kawe jijini Dar, kisha akatoa sadaka ya shukrani kwa
Mungu aliyemwezesha kutwaa tuzo hiyo.
Mbali na sadaka hiyo, Lulu akiwa kanisani hapo, aliombewa na
kufungukia kuokoka, jambo lililoibua shangwe kubwa za kumrudishia Mungu
sifa na utukufu miongoni mwa waumini wa kanisa hilo.
TAMKO LA LULU
Katika tamko lake baada ya zoezi hilo kanisani hapo, Lulu alisema:
“Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu pamoja na baba yangu (Michael Kimemeta) na mama yangu (Lucresia Karugila).
“Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu pamoja na baba yangu (Michael Kimemeta) na mama yangu (Lucresia Karugila).
“Sijutii kuokoka kwangu na hata wakisema vyovyote I don’t care (mimi sijali) ilimradi namuomba Mungu na mambo yangu yanaenda.”![lULU mUNGU](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_v4B6WVAISc90rDJ4Zfuerm20OoFBYP9V0xPUuk5vu2vPq0njMTJ9uRYUWxjynjv82tmXaPr8HfK26cpDw6JLMzvAvSveR9OUNGNw9ZwOuGuCi-N4DzKYzxrKkYw4wVHRnZm-L1zI_zkzy9=s0-d)
…..Akiwa na Biblia.
KILICHOFUATIA SASA
Mapema wiki hii, Lulu aliibua mjadala mzito miongoni mwa baadhi ya waumini hao wanaotumia mitandao ya kijamii na wale waliokutwa na Ijumaa kanisani hapo kufuatia picha zake chafu za nusu utupu alizoziachia mitandaoni baada ya kuzipiga ufukweni zikimuonesha akiwa amevaa nguo za ndani za bikini na sidiria huku sehemu kubwa ya maungo yake nyeti ikiwa wazi.

PICHA ZAIBUA GUMZO KANISANI
Kwa mujibu wa waumini hao wa Makuti-Kawe, picha hizo ziliibua gumzo
kubwa kanisani hapo wakistaajibishwa na kitendo alichokifanya Lulu
ambacho ni kinyume na maadili ya kanisa.
“Kiukweli jambo alilolifanya Lulu ni aibu, wakati mwingine tunashindwa kukubali pale anaposema ameokoka kutokana na matendo yake, anastahili kukemewa ili aache mara moja na akae kwenye mstari wa ulokole.

“Kwanza hapa kwetu hakuna muumini mlokole anayethubutu kupiga picha
za ajabu kama hizo maana ni kinyume kabisa na kanisa letu,” alisema
mmoja wa waumini hao akiungwa mkono na wenzake waliokuwa wakizungumza na
gazeti hili ndani ya viunga vya kanisa hilo.
“Kwanza Mtume Ndegi kama ameziona au akioneshwa zitamsikitisha sana
maana ni mtu anayesisitiza usafi wa mioyo na mwili,” alisema muumini
mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Jonas na kuongeza:
Moja ya picha zilizomletea utata.
“Itabidi kama Lulu atafika kanisani Jumapili (ijayo) aitwe ili
aombewe maana inawezekana alipitiwa na shetani anayetakiwa kukemewa kwa
nguvu zote.
LULU ATOA UTETEZI WA KUSHANGAZA
Kufuatia ishu hiyo kuwa kubwa kanisani hapo, Ijumaa lilimtafuta Lulu na
kumsomea ‘mashtaka’ yake ambaye alipopatikana alielezwa hoja za waumini
kuwa alichokifanya ni kinyume na maadili ambapo katika hali ya
kushangaza, hakuonesha kushtushwa na kudai hakuna tatizo kwa kuwa
hajapiga kanisani.
“Kwani cha ajabu ni nini hapo? Kwani wameona hizo picha nimepiga kanisani? Kama mnaona hapo ni kanisani sawa, labda ningekuwa nimepiga kanisani lakini sivyo,” alisema Lulu kwa kifupi kisha akakata simu.

MTUME NDEGI ASAKWA
Baada ya kutoridhishwa na majibu ya Lulu yaliyojaa viulizo, gazeti hili
lilifanya juhudi za kumtafuta Apostle (Mtume) Ndegi wa kanisa hilo ili
kumsikia anazungumziaje suala hilo?
Hata hivyo, juhudi hizo ziligonga mwamba, badala yake simu yake ilipokelewa na mmoja wa wasaidizi wake (jina lipo) na kufunguka kuwa, kitendo alichofanya Lulu si sawa lakini atabadilika neno litakapomkolea.

“Ila sisi hatuwezi kumlazimisha mtu kukaa kwenye mstari kutokana na
mambo yake binafsi kwani siku hadi siku anavyozidi kuja kwenye ibada
neno linavyozidi kumkolea mtashangaa amebadilika kabisa na kuacha yote
hayo, tunaamini hivyo,” alisema mtumishi huyo akiomba kutotajwa gazetini
kwani hana mamlaka hiyo.
SI MARA YA KWANZA KWA LULU KUOKOKA
Tangazo la sasa la kuokoka la Lulu si la mara ya kwanza kwani aliwahi
kufanya hivyo baada ya kukutwa na mkasa wa kifo cha aliyekuwa staa wa
sinema za Kibongo, Steven Kanumba ambaye pia alikuwa mwandani wake.
Note: Only a member of this blog may post a comment.