V ideo Queen na Mtangazaji wa Runinga, Gifty Stanford ‘Gigy Money’ juzikati alifakamia pombe kali na kujikuta akilewa tilalila hadi kuzimika ndani ya klabu moja iliyopo kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar.
Binti huyo asiyeishiwa na vituko alinaswa na mapaparazi wetu akiwa kwenye hali hiyo Jumatatu liyopita (Jumatatu ya Pasaka) ambapo awali alionekana akinywa pombe kali huku akivuta sigara. Baada ya kupombeka kwa muda mrefu huku akionekana kama aliyekuwa na mawazo mengi, taratibu mdada huyo aliyejaaliwa shepu alianza kupoteza ‘netiweki’.
Baada ya muda mfupi, alifika dada mmoja aliyeonekana kujuana na Gigy (inaonekana alipigiwa simu) ambapo alimchukua kwa kumkokota kisha akampakiza kwenye Bajaj wakaondoka.
Siku moja baada ya tukio hilo, Ijumaa lilimpigia simu Gigy Money na kumuuliza kulikoni amekuwa na tabia ya kulewa hadi kuzimika alipopatikana alijibu: “Ni maisha yangu, haina haja kunifuatilia.”
Note: Only a member of this blog may post a comment.