Mpenzi msomaji, baada ya wiki iliyopita kufikia tamati kwa simulizi
ya Mwanamuziki Ambwene Yessaya ‘AY,’ leo tunamleta kwenu mchekeshaji
maarufu Bongo kutoka Kundi la Mizengwe, Mkwere.
Hemedi Khalifan Maliyaga ‘Mkwere’
Basi ungana naye katika simulizi halisi ya maisha yake tangu alipozaliwa mpaka alipofikia.
“Jina langu halisi ni Hemedi Khalifan Maliyaga jina maarufu la kutafutia ugali ni Mkwere. Nilizaliwa mwaka 1981 Kata ya Ngerengere mkoani Morogoro nikiwa mtoto wa mwisho kati ya watoto watatu wa familia ya Mzee Khalifan Hassani Maliyaga na mama Mariamu Epate (mama yangu alikuwa ni shombeshombe wa Kihindi na Kibongo).
“Watanzania hatuna itikadi za kuulizana makabila kwa sababu sisi ni wa moja ila mimi ni Mkwere, nilianza shule ya chekechea pale maeneo ya Tandale CCM jijini Dar miaka ya 90. Baadaye niliendelea na darasa la kwanza mwaka 1991, Shule ya Msingi Mugabe, Shekilango, Dara. Kiukweli nilikuwa mtundu sana shuleni, tangu nikiwa mdogo nilikuwa napenda sana michezo ya kuigiza na hata walimu wangu walipenda sana kunishirikisha hasa kila kipindi cha wanafunzi wa darasa la saba wanapo-maliza masomo yao ya mwisho, kipindi kile tulikuwa tunaita ‘elowai’.
“Naweza kusema kuwa utundu wangu, kwangu ulikuwa ni wa faida kwani uwezo wangu hauku-jificha kabisa, nilikuwa siyo mtu wa kuona aibu, nilikuwa ni mwana
funzi ninayejiamini sana, nisiyeona tatizo kusimama mbele ya wanafunzi wenzangu hata kama watakuwa wengi kiasi gani.
“Nakumbuka mwaka 1994 moja ya sherehe ya elowai ilifanyika katika moja ya ukumbi maeneo ya Sinza, nilishiriki katika kucheza muziki na hata kuigiza, huwezi amini baada ya hapo walimu walinikubali sana na tangu siku hiyo nikawa sikosi kila sherehe zinazohusisha michezo ya sanaa. Naweza kusema hiyo ilizidi kunijenga sana kiakili na hata kifikra kwani nikazidi kuipenda sana sanaa na kiukweli sanaa yangu si ya kukurupuka kama wafanyavyo wengine, bali sanaa yangu ni ya kipaji cha ukweli kabisa ndiyo maana leo hii ninaweza kumchekesha mtu katika mazingira yoyote yale, iwe kuangalia, kuzungumza, kucheza nakadhalika.
“Ninaamini wakati ninaanza sanaa hii nilionekana kama mtukutu na mtundu f’lani lakini leo hii ndiyo kazi ambayo inaniweka mjini, ninaendesha gari mjini kwa sababu ya sanaa yangu. Mpenzi msomaji hujachelewa anza leo kujichunguza ni nini ambacho unaweza kukifanya kwa ufasaha haijalishi haujasoma, hauna pesa, au uko katika mazingira gani, ukikipata jaribu kuangalia ni namna gani unaweza kuishi au kuendesha maisha yako kwa hicho kipawa kilichowekwa na Mungu ndani yako.
“Ila usije ukakurupuka kwa kutaka kufanya kitu ambacho haukupewa na Mola na kama ukijidanganya ukakurupuka basi subiri kushindwa kwa sababu si kitu sahihi kilichopandikizwa ndani yako.”
Msomaji wa Mjue Huyu, makala haya ndiyo yanaanza utajua na kujifunza vitu vingi sana katika maisha ya Mchekeshaji Mkwere.

Note: Only a member of this blog may post a comment.