Aunt Ezekiel
BONIPHACE NGUMIJE NA MAYASA MARIWATA
Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: MAMA aliyejitambulisha kuwa ni mama mzazi wa dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’ Moses Iyobo, amefungukia habari iliyozagaa mitandaoni kuwa mwanaye ameachana na mzazi mwenziye, mwigizaji Aunt Ezekiel kwa kusema habari hizo si za kweli.

Mapema wiki hii, kwenye mitandao
mbalimbali ya kijamii, iliandikwa kuwa Moses amemwaga Aunt na kuamua
kuondoka nyumbani walipokuwa wakiishi na Aunt maeneo ya Mwananyamala-Kwa
mama Zakaria.
Mara baada ya kupata habari hizo
kusambaa, wanahabari wetu walimtafuta Aunt bila mafanikio katika simu
yake ya mkononi ndipo walipoamua kufunga safari hadi kwenye nyumba hiyo
wanayoishi Aunt na Iyobo.
Moses Iyobo na mpenzi wake, Aunt Ezekiel
Moses Iyobo na mpenzi wake, Aunt Ezekiel
Walipofika, waligonga geti ambapo
alitoka mama huyo aliyekataa kujitambulisha jina lake lakini akasema
yeye ni mama yake Iyobo na kufunguka kwa kirefu kuhusu taarifa hizo za
kuachana kwa mwanaye na Aunt.
“Hizo habari hata mimi nimezisikia.
Hazina ukweli wowote. Watu tu wanajaribu kutengeneza uzushi wao kwa
maslahi yao wanayoyajua wenyewe.
“Hawajaachana. Ingekuwa kuna ukweli
kuhusu habari hiyo, hata mimi usingenikuta hapa. Nipo hapa kwa sababu
mkwe wangu na mwanangu wako pamoja sema tu kwa sasa mwanangu Iyobo
amesafiri nje ya nchi lakini wapo vizuri,” alisema mama huyo.
Mapaparazi wetu walipoomba kuzungumza na
Aunt kuhusiana na habari hizo, mama huyo alisema haiwezekani kwa kuwa
amelala hivyo akaomba atafutwe siku nyingine.
Note: Only a member of this blog may post a comment.