Staa wa Bongo Fleva, Herry Samir ‘Mr Blue‛ siku ya harusi yake.
KWENU mastaa wa Bongo Fleva, Herry Samir ‘Mr Blue‛ na Ebrahim Mussa ‘R.O.M.A‛, habarini za siku Maisha mapya ya ndoa yapoje? Kuna utofauti au mambo ni yaleyale? Mkitaka kujua afya yangu, mimi niko fiti. Kama kawa, naendelea kupambana katika eneo langu na ninamshukuru Mungu maisha yanazidi kusonga, huenda na mimi siku moja mkasikia nimeoa. Umri unasogea kwa hiyo lazima tujiandae kwa suala hilo.Nimewakumbuka leo kupitia barua nzito, maana bahati mbaya hata kwenye harusi zenu sikuweza kuhudhuria kutokana na majukumu niliyokuwa nayo.
Lakini yote kwa yote, nina imani kila kitu kilikwenda sawa, mmeanza maisha ya ndoa. Ndugu zangu, natambua kila mmoja wenu amepitia changamoto zake hadi kufi kia hatua hiyo. Blue najua Waheeda mmetoka mbali, R.O.M.A pia, Nacy mmetoka mbali. Mmeishi kwenye uchumba muda mrefu. Mmesomana tabia vya kutosha hivyo mna kila sababu ya kupongezwa.
Nawapongeza kwa sababu wapo wasanii wa Bongo Fleva ambao pengine mmewakuta kwenye gemu au hata wa umri wenu lakini mpaka leo hawana mawazo ya kuoa. Kina Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA‛, Joseph Mbilinyi ‘Sugu,‛ Ambwene Yessaya ‘AY,‛ John Saimon ‘Joh Makini‛ na wengine kibao bado hawajafi kia hatua hiyo.
Muziki upo lakini maisha binafsi pia yapo! Kutoingia kwenye ndoa kwa kijana aliyefi kisha miaka 30 na zaidi si ishara nzuri maana kinaleta tafsiri ambayo si njema sana. Huwezi kuishi peke yako miaka yote. Huwezi kuwa mhuni au mtu wa kula bata, kula hotelini na kwenda klabu kila siku. Kuna wakati lazima maisha yabadilike.
Uishi kama baba wa familia. Uwe na watoto. Uwasomeshe na uwatimizie mahitaji yao ya kila siku. Hayo ndiyo majukumu. Hakuna namna, kwa mpango wa Mungu lazima uyaingie ili kukamilisha maisha ya hapa duniani hata kama baadhi ya watu wanaamini si lazima kuoa au kuolewa.Hakuna sababu ya kuogopa, kuoa au kuolewa hakuwezi kukupotezea soko la muziki.
Suala la msingi ni kujiwekea mikakati mizuri ya kufanya muziki unaoendana na umri wako na utapata mashabiki kama kawaida.Mifano ipo mingi tu hata katika nchi za wenzetu ambao wametangulia kufanya muziki. Kina Jay Z na Beyonce wameishi kwenye ndoa japo ya siri lakini kwa miaka mingi na wanaendelea kutusua.
Niwasihi Blue na R.O.M.A msiyumbishwe na kelele za watu, ishini mnavyotaka na ninaamini mtaendelea kufanya vyema kwenye muziki na ndoa zenu zitazidi kupata baraka tele. Nawatakia kila lakheri, mimi ni ndugu
yenu;
Erick Evarist
Note: Only a member of this blog may post a comment.