Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ akipiga mtungi huku akijilipua na fegi.
Na Gladness Mallya, RISASI mchanganyiko
DAR ES SALAAM: Mwanadada asiyeishiwa matukio mjini,
Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ hivi karibuni alinaswa akigida bia na kuvuta
sigara asubuhi na mapema, akionekana kukaidi agizo la Rais John Joseph
Magufuli la kuwataka watu kuachana na tabia ya kunywa pombe saa za kazi.
Paparazi wetu alimnasa Aunty Lulu ndani ya baa ya Mango Garden,
Kinondoni jijini Dar ambapo alikuwa anakunywa bila wasiwasi huku
akishushia na kuvuta sigara hali iliyosababisha watu kumkodolea macho
huku wengine wakijadili amekuwaje siku hizi kulewa asubuhi tena muda wa
kazi.
“Jamani Aunty Lulu amebadilishwa na nini maana siyo mara ya kwanza
kumuona anakunywa muda wa kazi huku akivuta sigara kwa wingi, hilo pakti
la sigara analotembea nalo atamaliza kuvuta sasa hivi,” alisema mtu
mmoja aliyekuwa akinywa supu katika baa hiyo, wakati msanii huyo
akipuliza moshi bila woga.
Baada
ya paparazi wetu kumpiga picha za kutosha, alimfuata Aunty Lulu na
kumuuliza kulikoni kunywa pombe muda wa kazi na kukiuka maagizo ya rais
ambapo alisema;
“Unajua siku hizi nafanya kazi ya biashara ya kusafiri mikoani hivyo siku ambayo napumzika kama hivi nakunywa kuanzia asubuhi ili kutuliza mawazo, hizi sigara navuta ili kupunguza mwili maana niliambiwa na watu kwamba zinapunguza unene, nataka kurudi kuwa miss kama zamani.
“Unajua siku hizi nafanya kazi ya biashara ya kusafiri mikoani hivyo siku ambayo napumzika kama hivi nakunywa kuanzia asubuhi ili kutuliza mawazo, hizi sigara navuta ili kupunguza mwili maana niliambiwa na watu kwamba zinapunguza unene, nataka kurudi kuwa miss kama zamani.
“Agizo la rais sijalisikia bado lakini najua hapa sijavunja sheria
maana si unajua kila mtu ana siku yake ya mapumziko na mimi leo niko
mapumziko ndiyo maana nakunywa saa hizi.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.