TAKRIBANI watu watano wameuawa wakati wa ufyatuaji wa risasi
uliotokea karibu na mji wa Pittsburg uliopo kwenye Jimbo la Pennsylvania
nchini Marekani.
Maofisa wa polisi wameeleza kuwa watu waliokuwa na silaha walifyatua
risasi kwenye sherehe moja ambapo pia watu wengine watatu walijeruhiwa.
Watu wanne kati ya waliouawa walikuwa ni wanawake huku watu waliofanya mauaji hayo wakiwa bado hawajafahamika.
Misururu ya mauaji kwa kutumia bunduki imechangia suala la umiliki wa bunduki kuwa mjadala mkubwa nchini Marekani.
Watu wanne walikufa eneo la mkasa huku mmoja akiaga dunia
alipofikishwa hospitalini. Wanaume wawili waliojeruhiwa wako katika hali
mahututi.
Chanzo: BBC
Note: Only a member of this blog may post a comment.