Leo March 10 2016 Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), Saed Kubenea amehitajika
polisi kwa tuhuma za kuhusika na vurugu wakati uchaguzi
huo ulipoahirishwa February 27 2016. Saed Kubenea ameelezea kuhusiana na
wito huo wa polisi kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo na amesimulia
ilivyokuwa…
’Nimefuatwa
na askari kama sita wakiniambia kwamba niko chini ya ulinzi
ninahitajika makao makuu ya polisi Dar es salam nikahoji kosa langu ni
nini? wakasema nikajibu tuhuma juu ya vurugu zilizotokea katika uchaguzi
wa Meya wa Dar es salaam‘:-Saed Kubenea
’Mimi
nilifika makao makuu polisi kuwasilisha malalamiko juu ya amri
iliyotolewa kwamba uchaguzi ule uzuiliwe, niliwathibitishia Polisi
kwamba amri ile ilikuwa haramu na ilikuwa imeexipire kwa hiyo ni lazima
wachukue hatua za kisheria dhidi ya wahusika‘:-Saed Kubenea
Hii ndio video yake….
Note: Only a member of this blog may post a comment.