Serikali
ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imepokea msaada wa fedha
kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 5 kwaajili ya kusupport mamlaka ya
mapato katika kuongeza kipato nchini na kuongeza nguvu katika kuzuia
mianya ya ukwepaji kodi kwa Watanzania.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk Ashatu Kijaji amesema>> ‘Serikali
ya Kifalme ya Norway imetoa msaada kwa Tanzania katika kuimarisha
ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha kwamba tunaweza kuzuia wanaokwepa
kulipa kodi‘
‘Wizara
ya fedha tunataka kuondoka kutoka katika bajeti ya utegemezi na kwenda
katika bajeti ya kujitegemea, lakini hatuwezi kufika huko bila
kuimarisha ukusanyaji wa mapato‘
‘Kwahiyo
tunaishukuru sana Serikali ya Norway kwa msaada huu na pia tunawaahidi
tutazitumia vizuri katika kuimarisha mamlaka yetu ya mapato na kazi zake
kwa ujumla ‘
Note: Only a member of this blog may post a comment.