Headline
zilizoongoza kwenye magazeti ya Tanzania March 14 2016 ni kuhusu uteuzi
wa wakuu wa mikoa nchini, miongoni mwa waliozikamata zaidi headline hizo
ni aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.
Sasa baada ya hayo yote, Paul Makonda
akatangazwa kwamba ndio Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es salaam, wakati
akitangazwa hakuwa akijua kwamba atatangazwa kuwa Mkuu wa Mkoa.
‘Leo
nilikuwa natimiza mwaka mmoja tangu kuteuliwa kwangu kuwa Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, pia nilienda kuzindua na kuweka jiwe la msingi
kwenye ujenzi wa jengo laupasuaji katika hospitali ya Mwananyamala‘
Alizipata vipi taarifa za kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa? ‘Sina
uhakika zaidi kwasababu mtu hata akipiga simu mimi nilikuwa najua ni
utani, lakini nilikuja kuamini baada ya kuliona jina langu kwenye
karatasi yenye nembo ya Serikali ‘ ;-Paul Makonda
Note: Only a member of this blog may post a comment.