Paul M akonda Dar es Salaam.
Na Waandishi Wetu, UWAZI
DAR ES SALAAM: Juzi Jumapili, Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ alitangaza wakuu wa mikoa wapya 26 wa Tanzania Bara na kuweka sura mpya 16 na kubakiza za zamani 10, huku baadhi ya wasomaji wa gazeti hili wakisema miongoni mwa hao, wapo ambao ni majipu na wanahitaji kutumbuliwa, Uwazi linashuka na habari yote.
MITANDAONI
Baada ya uteuzi huo, mijadala mikubwa ilizuka katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini huku kila kundi likielezea mtazamo wake.
“Rais Magufuli nusu amepatia lakini nusu amechemka. Hawa jamaa (wakuu wa mikoa), wapo ambao ni majipu ambao hawakustahili kupewa nafasi lakini mimi siamini kama wanaweza kuzitumikia vizuri nyadhifa zao,” alitupia mchangiaji mmoja kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook.
MITAANI PIA
Mbali na mitandaoni, wasomaji wa gazeti hili ambao wapo katika kona mbalimbali za nchi, walipiga simu chumba cha habari, wengine wakikutana na waandishi wetu na kueleza mitazamo yao kuhusu uteuzi wa wakuu hao wa mikoa.

Halima Dendegu, Mtwara.
WANAJESHI WASHANGAZA
“Mimi nimeshangazwa na wingi wa wanajeshi, wengine ni JWTZ, wengine polisi. Hivi anakusudia kuiweka nchi katika hali gani?” alihoji Abbas Aziz, mkazi wa Geita.
Wakati huyo akihoji hivyo, Jumanne Mrisho, mkazi wa Tabata ya Liwiti, Dar alisema: “Mimi nimefurahishwa na wingi wa wanajeshi. Hawa jamaa huwa hawana mchezo kazini, wana nidhamu ya hali ya juu.
“Nakumbuka hata enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliweka wakuu wa mikoa wengi wanajeshi, hasa kwenye mikoa iliyo mipakani mwa nchi na walifanya vizuri sana.”
MAKONDA KINARA WA GUMZO
Katika hali ya kushangaza, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda aliongoza kwa kuzungumziwa sana mitandaoni na mitaani huku hoja kubwa ikiwa ni ukubwa wa Mkoa wa Dar es Salaam aliopewa kuuongoza, umri wake na uzoefu katika kazi.
Wengi walionesha kuunga mkono uteuzi wa rais juu yake, hususan alivyokuwa akijituma katika kutimiza majukumu yake. Wengine walikumbushia hotuba ya rais aliyoitoa jijini Dar kwenye Maadhimisho ya Siku ya Sheria Duniani ambapo alisifu utenda kazi wake na kusema hadharani kuwa, watu wasishangae akipanda cheo.
“Makonda ana umri mdogo, anaweza kweli kuumudu Mkoa wa Dar es Salaam wenye changamoto nyingi za kiuongozi?” alihoji mmoja wa wachangiaji mtandaoni ambapo hata hivyo, alikumbana na upinzani mkali kutoka kwa wachangiaji wengi waliopongeza utenda kazi wake.
“Ni kipofu na kiziwi pekee ndiye asiyeweza kuona mchango wa Makonda katika masuala ya uongozi kwa muda mfupi aliopewa Wilaya ya Kinondoni.
“Katika nyakati kama hizi ni ajabu kuhoji umri wa mtu bila kuangalia uwezo alionao. Kizazi hiki kinataka kuongozwa na akili mpya zenye uwezo wa kuendana na ulimwengu wa sayansi na teknolojia,” alisema Dickson Mwambenja, mkazi wa Katumba, Tukuyu, Mbeya.
WANANCHI WAGAWANYIKA
Ukiachilia mbali Makonda na wanajeshi waliochukua mjadala mkubwa, wakuu wa mikoa wengine hawakuwa salama kutokana na kuungwa mkono au kupingwa, jambo ambalo liliifanya Timu ya Gazeti la Uwazi kuanza kupekua wasifu wa kila mmoja.
PAUL MAKONDA, DAR ES SALAAM
Ni kijana mwenye msimamo. Alitokea Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM), akateuliwa na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni hadi juzi alipopewa ukuu wa mkoa.

Akiwa Kinondoni, alisimamia utatuzi wa migogoro ya ardhi, ujenzi wa shule za sekondari, upatikanaji wa huduma bora za afya, kuhamasisha vijana kuhusu kujiajiri na kutoa fursa kwa walimu wa Dar kupanda daladala bure.
ANNA KILANGO MALECELA, SHINYANGA
Pichani ni mwanamke mpambanaji, amewahi kuwa mbunge machachari ndani ya bunge akiwakilisha Jimbo la Same Mashariki (CCM), Mwenyekiti wa UWT, Kinondoni na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi (Serikali ya JK) nafasi ambazo alizitumikia kwa ufanisi.
AMOS MAKALLA, MBEYA
Makalla amelelewa na CCM, amewahi kushika wadhifa nyeti wa Katibu wa Uchumi wa chama hicho kabla ya kuwa Mbunge wa Mvomero, Morogoro. Akawa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, baadaye akawa Waziri wa Maji (utawala wa JK).
Alipoanguka ubunge, akateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambako alikuwa gumzo kwa uchapakazi wake.
ZELOTHE STEVEN, RUKWA
Ni Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Tanzania. Amewahi kushika nyadhifa mbalimbali. Anasifika kwa umahiri wake wa kupambana na majambazi na kudhibiti madawa ya kulevya. Baada ya kustaafu, akachaguliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mara.

GODFREY ZAMBI, LINDI
Amewahi kuwa Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mbunge wa Mbozi Mashariki (CCM) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya. Pia ameshakuwa kwenye kamati mbalimbali za bunge ambapo misimamo yake ilikuwa ya kutetea wanyonge.
AGGREY MWANRI, TABORA
Atakumbukwa kwa umahiri wake katika kujibu maswali bungeni alipokuwa Naibu Waziri wa Tamisemi na Mbunge wa Siha. Alitajwa kuwa waziri mwenye uelewa mpana wa mambo.
DK. STEVEN KEBWE, MOROGORO
Amewahi kuwa Mbunge wa Serengeti (CCM) pia akahudumu katika nafasi ya Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii. Ni mwanasiasa mpole na mfuatiliaji wa mambo ya kijamii.
ANTONY MATAKA, SIMIYU
Ametokea kwenye ukuu wa wilaya akimwakilisha rais katika Wilaya ya Mvomero. Anatajwa kuwa ni miongoni mwa wakuu wa wilaya vijana waliofanya vizuri katika utumishi wa umma.
MARTINE SHIGELA, TANGA
Amewahi kuwa Katibu Mkuu wa UV-CCM- Taifa kabla ya kuteuliwa kuwa msaidizi wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kwenye masuala ya siasa. Ni miongoni mwa wanasiasa vijana machachari nchini ndiyo maana JPM amempa Mkoa wa Tanga.
JORDAN RUGIMBANA, DODOMA
Alianza kupata jina akiwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Dar. Akaja kupelekwa Kinondoni kabla ya kuhamishiwa Wilaya ya Morogoro Mjini na baadaye kupandishwa cheo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwa kuzingatia sifa za alikopitia.

Alianza kusikika akiwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam enzi za Abass Kandoro lakini nafasi yake ilikuwa ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi. Wakazi wa Dar watamkumbuka kwa alivyokuwa akipambana na ugonjwa wa kipundupindu na kusimamia miundombinu ya jiji.
MAGESA MULONGO, MARA
Huyu jina lake lilianza kusikika akiwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, akapanda cheo kwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, baadaye Mwanza ambapo Rais JPM amemwamini kwa kumpeleka Mara. Ni kiongozi mwenye msimamo asiyependa kuyumbishwa.
JOHN MONGELLA, MWANZA
Ana historia ndefu katika ulingo wa siasa. Nyota yake ilianza kung’aa baada ya kuteuliwa na JK kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma. Baada ya hapo akapelekwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera akichukua nafasi ya Fabian Masawe. Kiasili ni mpole, asiye na pupa. Kagera watamkumbuka kwa tabia yake ya kutokaa ofisini akitembelea wananchi kuangalia matatizo yao.
DAUDI NTIBENDA, ARUSHA
Ni miongoni mwa wakuu wa mikoa waliobaki kwenye nafasi zao. Awali aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu, baadaye akahudumu ukuu wa Wilaya ya Arusha kabla ya kupanda na kuwa mkuu wa mkoa huo.
JOEL BENDERA, MANYARA
Ana historia ndefu sana kwenye masuala ya michezo. Amewahi kuwa mchezaji na Kocha wa Timu ya Taifa kwenye miaka ya 80. Pia amewahi kuwa Mbunge wa Korogwe Mjini (CCM), baaye akawa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Alipoanguka ubunge, akapewa ukuu wa Mkoa wa Morogoro, baadaye Manyara ambako amebaki.

EVARIST NDIKILO, PWANI
Ni miongoni mwa wakuu wa mikoa waliobakizwa kwenye vituo vyao vya kazi. Lakini kabla ya kuwa Pwani, alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Ana msimamo wa kutetea analoliamini.
SAID MWAMBUNGU, RUVUMA
Historia inambakiza Ruvuma kwa awamu nyingine kwani tangu mwaka 2011, aliteuliwa kuwa mkuu wa mkoa huo. Rais Magufuli amemuona anafaa kuendelea kuhudumu katika nafasi hiyo.
LUTENI MSTAAFU CHIKU GALAWA, SONGWE
Baada ya kustaafu jeshi, aliteuliwa kuuongoza Mkoa wa Tanga, baadaye akahamishiwa Mkoa wa Dodoma kabla ya juzi, Rais Magufuli kumpeleka Mkoa wa Songwe (mpya) uliogawanywa kutoka Mkoa wa Mbeya. Anasifika kwa uchapakazi wa bila kujali muda.
DK. REHEMA NCHIMBI, NJOMBE
Amebaki kama Chiku Galawa. Ni mwanamke mpambanaji, alitokea Mkoa wa Dodoma. Baada ya kutua Njombe, Magufuli akamwona anatakiwa aendelee kuuweka sawa mkoa huo ambao ulitokana na Mkoa wa Iringa.
AMINA MASENZA, IRINGA
Huyu amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa tangu awamu iliyopita ya Rais Mstaafu Kikwete. Utenda kazi wake, Magufuli ameona aendelee kuhudumu mkoa huo.
HALIMA DENDEGU, MTWARA
Amewahi kuwa mwakilishi wa Rais Kikwete kwenye Wilaya za Kilosa, Morogoro Mjini, Morogoro Vijijini na Mvomero. Mwaka 2013, alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga kabla ya kupelekwa Mtwara ambako naye amebaki.
KUNA HAWA
Wengine ambao historia zao za nyuma haziko wazi sana ni Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga (Geita), Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu (Kagera), Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Muhuga (Katavi), Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga (Kigoma) na Mhandisi Methew Mtigumwe (Singida).
IKULU YASIFU
Licha ya kuwepo kwa manenomaneno kuhusu uteuzi huo, Ikulu imesema kuwa imejiridhisha kwamba, walioteuliwa wanakidhi sifa na matakwa ya rais.
“Hakuna jipu katika hawa wateule. Rais alichukua muda kuwatangaza ili kuwafuatilia kwanza kuona sifa zao kama zinaendana na kasi yake. Ana uhakika watafanya kazi aliyowatuma, atakayeshindwa atatumbuliwa,” alisema afisa mmoja wa ikulu ambaye hakupenda jina lake litajwe.
KWENU WASOMAJI
Gazeti la Uwazi linaamini kuwa watumishi wote wa serikali wameajiriwa na wananchi hivyo gazeti linatoa nafasi kwao kutoa maoni kuhusu kukidhi au kutokidhi kwa wateule hao. Mapendekezo na mitazamo yao itapelekwa ikulu kwa Rais Magufuli.
Kwa wanaotaka kuwasilisha walichonacho, wawasiliane na gazeti hili kwa simu 0753 715 779.
Note: Only a member of this blog may post a comment.