Tuesday, March 8, 2016

Anonymous

Mnorway Amgongea DOGO JANJA Ngoma Mbili

Carl Hovind  (1)
Norway, Carl Hovind
Andrew Carlos
BAADA ya kufanya poa Ngoma ya My Life, staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ amefunguka kuwa prodyuza aliyemtengenezea ngoma hiyo ambaye ni raia kutoka Norway, Carl Hovind anahusika pia katika ngoma yake ya pili.
Akichonga na Showbiz Dogo Janja alisema kuwa, Ngoma ya My Life video yake inatarajiwa kuachiwa siku yoyote kuanzia leo na kwamba mashabiki wajiandae kumsikia katika ngoma nyingine iliyopikwa na Carl.
janja
Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’.
“Video ya My Life ipo tayari imetayarishwa na Hanscana na inatarajiwa kuachiwa muda na siku yoyote, nimpe tano za kutosha prodyuza aliyeipika ngoma hiyo, Carl Hovind anajua ndiyo maana amenitengenezea tena ngoma nyingine ambayo jina lake litakuwa sapraizi kwa mashabiki,” alisema Dogo Janja.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.