Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,
akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya Hindu Mandal
Jijini Dar es Salaam kuelezea maendeleo ya afya yake.
Akiwapungia mkono kama ishara ya kuwaaga wanahabari na wananchi waliofika kumjulia hali.
Baada ya katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif
kurejea kutoka India alipokuwa anafanyiwa upasuaji wa Mgongo na kwa
mujibu wa Daktari wake upasuaji ulifanikiwa na aliporejea alikuwa na
afya njema na akapumzika Zanzibar.
Leo March 8 2016 Maalim Seif Sharif amethibitisha
jana hali yake ilibadilika ghafla akiwa uwanja wa ndege Zanzibar,
alipata kizunguzungu kikali ikabidi asaidiwe kupelekwa kupanda ndege
kutoka Zanzibar mpaka Dar es salaam na kisha kulazwa hospitali na
leo ameyazungumza haya…
“Nilipofikishwa hapa walikuwa
washajitayarisha wamenipokea vizuri sana wakaanza kufanya uchunguzi wao
na baada ya muda kama saa mbili tatu hali ikarudi ikatengamaa, nikalala
salama usingizi mzuri na nimeamka salama asubuhi nimefanya mazoezi kwa
miguu yangu mwenyewe na ninatembeatembea kwa miguu yangu mwenyewe, hali
sasa hivi ni nzuri kama kama kawaida” alisema Maalim Seif Sharif
Daktari wa Maalim Seif Sharif, Omary Mohamed Suleiman amethibitisha pia kuwa afya ya kiongozi huyo kuwa ni njema na muda wowote madaktari watamruhusu..
“Hakuna kubwa lililoonekana kila
kitu kipo sawa, isipokuwa inaonekana ni hali ya uchovu alihitaji
mapumziko zaidi na baada ya kufika hapa Hospitali madaktari baada ya
uchunguzi wao wakaona bora abakie hospitalini wazidi kumuangalia mpaka
kesho yaani leo mpaka sasa hivi hali imeenda vizuri tunategemea wakati
wowote ataruhusiwwa kwa mujibu wa madaktari,” alisema Omary Mohamed
Suleiman
(Picha na Salmin Said, OMKR)
Note: Only a member of this blog may post a comment.