Maisha yanafurahisha sana wakati mwingine. Na kwakweli vitu vidogo
vidogo vinavyochekesha na kushangaza, huifanya dunia isiwe sehemu
inayoboa.
Unajua kwa mfano mtu ukishazoea kushindwa, automatically akili yako
inajitengenezea imani kuwa wewe ulizaliwa kushindwa tu. Ni mbaya zaidi
imani hiyo ikitoka kwenye hatua binafsi na kuingia kwenye hatua ya
kitaifa.
Kushindwa kwetu kwenye michezo ya kimataifa kwa mfano, kumewafanya
watanzania wengi wajiaminishe kuwa Tanzania ni wa kushindwa siku zote.
Tumejikatia tamaa na kuikubali hali hiyo.
Tumejiaminisha kuwa sisi ni wa
hivyo hivyo kiasi ambacho ikitokea mtu au kundi limefanya tofauti,
inakuwa ngumu kuamini.
Nimesikitika sana baadhi ya watanzania wanaoushuku ushindi wa
Elizabeth ‘Lulu’ Michael kwenye tuzo za AMVCA 2016 zilizofanyika Lagos,
Nigeria. Mbaya zaidi ni pale ambapo wapo wanaoaminishwa kuwa ushindi wa
Lulu umetokana na nguvu za giza. Yes, huenda bado hujasikia, lakini
uvumi huo upo umeandikwa Instagram:
Inasikitisha kumtishwa msichana huyo skendo kubwa kama hii. Japo
ujumbe wake umefutwa tayari, Lulu ameonekana kuumizwa na kuamua kusema
yake:
Katika kipindi ambacho watanzania wote tunapaswa kumpongeza na kumpaka kama tulivyofanya kwa kumuandalia mapokezi ya kishujaa ambayo yamewashtua hadi Afrika Magharibi, wapo watu wachache wanaojaribu kumkatisha tamaa. Kwanini watanzania tujichukulie poa hivi? Leo hii imefika hatua kwamba tasnia ya muziki Tanzania ni ya tatu kwa ukubwa Afrika, baada ya Nigeria na Afrika Kusini. Tunaweza kupata umaarufu huo kwenye filamu pia. Waigizaji kama Lulu, Wema na wengine wenye uelewa mzuri wa lugha iliyokuja kwa meli (kimombo), wanaweza kuitangaza Tanzania kama wakiandaliwa mazingira mazuri.
Na siku zote biashara ya showbiz hufanikiwa kutokana na support inayopewa na mashabiki. Support hiyo hiyo ndiyo iliyompa ushindi Lulu kwakuwa mashabiki wake na wengine wenye uzalendo na nchi yao walimpigia kura. Kura ndizo zilizompa ushindi Lulu na sio uchawi! Sasa hizi shaka zinatoka wapi? Tujiamini watanzania wenzangu.
Na siku zote biashara ya showbiz hufanikiwa kutokana na support inayopewa na mashabiki. Support hiyo hiyo ndiyo iliyompa ushindi Lulu kwakuwa mashabiki wake na wengine wenye uzalendo na nchi yao walimpigia kura. Kura ndizo zilizompa ushindi Lulu na sio uchawi! Sasa hizi shaka zinatoka wapi? Tujiamini watanzania wenzangu.
-via Bongo5
Note: Only a member of this blog may post a comment.