Sony italipa dola milioni 750 kwa familia na waangalizi wa kazi za Michael Jackson baada ya kununua hisa za kampuni waliyomiliki pamoja
Jackson alikuwa akilimiki 50% za hisa za kampuni ya Sony ATV Music Publishing kama sehemu ya ushirikiano wa kibiashara ulioanza mwaka 1995. Ununuzi huo utaipa haki Sony kumiliki karibu nyimbo milioni tatu zikiwemo za Beatles, Bob Dylan na Taylor Swift.
Hata hivyo dili hilo halihusishi nyimbo za Jackson.
Kampuni yake itaendelea kushikilia kazi zake kupitia Mijac Music, inayomiliki nyimbo zote zilizoandikwa na Jackson pamoja na EMI Music Publishing.
Makubaliano hayo yamedaiwa kusaidia kupunguza madeni yake yaliyosalia ya dola milioni 250 na kuwapa uhakika wa kifedha watoto wake watatu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.