Aliyekuwa mshindi wa Miss Dar City Centre 2014, Jihan Dimechk.
Na Andrew Carlos,RISASI mchanganyiko
SHINDANO la kusaka warembo lijulikanalo kama Miss Dar
City Centre linatarajiwa kuzinduliwa rasmi Jumamosi hii, Aprili 23 ndani
ya Ukumbi wa Golden Tulip jijini Dar.Akizungumza na Risasi Mchanganyiko mratibu wa shindano hilo, Nancy Joseph alisema ufunguzi huo ni maalum kwa ajili ya kuelekea katika shindano lenyewe litakalofanyika Mei 21, mwaka huu.
“Tutakuwa na wadau na wakurugenzi mbalimbali wa masuala ya urembo na lengo kuu ni kulizindua rasmi shindano hili,” alisema Nancy.
Mara ya mwisho kufanyika shindano la Miss Dar City Centre ilikuwa mwaka 2014 ambapo Jihan Dimechk aliibuka kidedea.Shindano hili limedhaminiwa na Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers.
Note: Only a member of this blog may post a comment.