Ikiwa leo ni Siku ya Wanawake Duniani,
mwanamitindo maarufu nchini, Jokate Mwegelo amesherehekea na kinamama
wajawazito na waliojifungua katika Hospitali ya Palestina Sinza, Dar kwa
kuwapa zawadi mbalimbali.
Akizungumza hospitalini hapo, Jokate
alisema ameamua kusherehekea na wanawake hao kwa kuwapa zawadi
mbalimbali kama vile viatu, dawa za meno kutoka kwenye kampuni yake ya
Kidoti kwa sababu leo ni siku muhimu sana kwa wanawake wote duniani
hivyo akaona siyo vyema kusherehekea peke yake.
“Nina furaha sana kwa siku ya leo kwani
ni muhimu kwetu sisi wanawake, nimeamua kugawana kidogo ninachopata kwa
hawa wanawake waliojifungua leo na wanaosubiri kujifungua. Hii yote ni
katika kuutambua umuhimu wa mwanamke duniani,” alisema Jokate.
PICHA/STORI: GLADNESS MALYA/GPL
Note: Only a member of this blog may post a comment.