Thursday, March 10, 2016

Anonymous

Fedha Ninazoringishia Instagram ni Feki – 50 Cent

50 Cent anadai kuwa fedha anazopost kwenye Instagram kiasi cha jaji kumtaka atoe maelezo ni feki.
Jaji Ann Nevins amemtaka 50 atokee kwenye mahakama ya masuala ya kufilisika Jumatano hii kuelezea picha hizo za Instagram. Moja ya picha hizo zinamuonesha rapper huyo akiwa amezungukwa na lundo la fedha zilizoandika neno ‘broke.’

Rapper huyo hata hivyo amesema fedha hizi sio halisi na kwamba hajaficha mali zake.
50 Cent, aliyezaliwa kwa jina Curtis Jackson III, alitangaza kufilisika baada ya mahakama kumtaka atoe dola milioni 7 kwa mwanamke aliyepost mkanda wake wa ngono mtandaoni.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.