STAA wa filamu Bongo, Yobnesh Yusuph
‘Batuli’ amesema miongoni mwa vitu vinavyomnyima furaha kipindi hiki ni
ndoa ya msanii wa filamu, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ ambayo inadaiwa
kuvunjika.
Akibonga machache na paparazi wetu
juzikati, Batuli alisema anawashangaa wanao shabikia ndoa hiyo kuyumba,
mbaya zaidi wengi wao ni wanawake ambao huenda nao siku moja yakawafika.
“Niliona jambo la heri Rayuu kuolewa,
sasa hizi figisu zinazoibuka zinanikosesha amani kabisa, kikubwa afuate
taratibu za dini kuhusiana na talaka hiyo,” alisema Batuli.

Note: Only a member of this blog may post a comment.