Saturday, February 20, 2016

Anonymous

VIDEO: Baada ya MADEE Kusikia Matusi ya Dogo JANJA Kwenye Ile Sauti ya Simu Iliyosambaa Aeleza Kinachofuata!

Juzi kati msanii wa bongofleva Dogo Janja alijikuta kwenye vichwa vya habari baada ya kuvujishwa kwa sauti yake kwenye maongezi ya kumtongoza msichana kwenye simu ambapo akajikuta ameilalamikia Tiptop Connection kwa kuchelewa kuachia nyimbo zake mpya ili kuuvunja ukimya wa zaidi ya miaka miwili. 

Kwenye hayo maongezi ya simu Dogo Janja alijikuta ametoa matusi kwa Tiptop na alikua huru kuongea mambo mengi sababu alijua ni maongezi ya kawaida ya simu na kwanza alikua hana idea hata kama yanarekodiwa, sasa Boss na kiongozi wa Janja ambaye ni Madee ameyasikia yale matusi na anatueleza mkasa mzima na kinachofuata kwenye video hii hapa chini.
Unaweza kuisikiliza sauti yenyewe ya maongezi ya simu ya Dogo Janja na Msichana aliyekuwa akimtongoza

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.