Tuesday, March 8, 2016

Anonymous

Baada ya Moshi wa Soko la Samaki Ferry Uliokuwa Unaingia Ikulu Kuwa Kero, Hili Ndilo Limetokea Leo!


Issue ya Moshi kutoka soko la samaki Ferry kuingia Ikulu lilichukua headline mwanzoni mwa mwaka huu, Moshi huo ambao unatokana na aina ya majiko yanayotumiwa na wauza samaki hao. 

Leo March 8 2016 Mkuu wa wilaya ya Ilala Isaya Mguluni kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, amezindua majiko 48 yanayotumia nishati ya gesi katika soko la samaki Ferry ili kupunguza moshi unaotokana na matumizi ya kuni ambao uliokuwa unaingia mpaka Ikulu. 

Awali Mkuu Huyo wa Wilaya alizindua bodi ya soko la samaki Ferry,  ambapo ilikuwa ni kilio cha muda mrefu kukosekana kwa Bodi hiyo tangu kuanzishwa kwa soko hilo. Bodi hiyo inaundwa na wajumbe 9 ambao watatekeleza majukumu yafuatayo
  • kufanyia kazi mapendekezo ya kamati ya soko 
  • kutoa miongozo mbalimbali kwa wadau wa soko juu ya taratibu zinazotakiwa kufuatwa ndani ya soko
  • kufanya shughuli kwa mujibu wa sheria ndogo hizi
  • kuidhinisha mapato na matumizi ya soko (bajeti).
  • kusimamia ulinzi na usalama wa soko
  • kuthibitisha uteuzi wa mkuu wa soko

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.