Friday, March 18, 2016

Anonymous

Baada ya Madaktari Kukataa, Amfanyia Upasuaji Dada’ke Akuta Mapacha [VIDEO]

Dead
Douala, Cameroon
Na Joe Dinga Pefok
WATU watano wamekamatwa wakituhumiwa kusababisha kifo cha mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Monique Koumate na watoto wake mapacha Jumamosi, iliyopita huko Douala, Cameroon.
Waliokamatwa ni mkunga wa hospitali hiyo, wakunga wawili, Mhudumu Mkuu wa chumba cha kuhifadhia maiti ‘Mortuary’ na mdogo wa marehemu Koumate.
Dead (3)
Taarifa za awali zilizotolewa na mashuhuda wa tukio hilo zinaeleza kuwa, mwanzoni Koumate alifikishwa hospitali akiwa katika hali mbaya akisaidiwa na mdogo wake aliyejulikana kwa jina la Agnes. Japo hali ya mama huyo ilikuwa mbaya alikuwa kwenye hatua za mwisho za kutaka kujifungua, wahudumu wa afya waliokuwa zamu walikataa kumsaidia kwa sababu hakuwa na pesa kwa ajili ya kulipia huduma hiyo. 

Agnes alijitahidi kuwasihi wahudumu hao wamsaidie dada yake kwani atawalipa baadaye kwa kuwa hakwenda na pesa lakini waliendeleza msimamo wao kwamba mpaka alipie kwanza gharama ndipo watamsaidia kumzalisha.

Kutoakana na kukoswa msaada, Koumate alifariki muda mfupi baadaye. Baada ya kuona dada yake ameaga dunia, Agnes aliwaomba tena wahudumu hao wamfanyie upasuaji marehemu ili kuwaokoa watoto waliokuwa tumboni ilihali walisikika kucheza, hivyo ikadhihirisha bado ni wazima. lakini wahudumu wale walisisitiza walipwe kwanza ndipo watoe huduma hiyo. Agnes alichukua jukumu la kuchana tumbo la marehemu dada yake ili aokoe wale watoto mapacha.
Dead (1)
Dead (2)
Agnes alijitahidi akamtoa mtoto wa kwanza akiwa amefariki, wa pili akawa mzima lakini baadaye naye alifariki.
Taarifa zingine kutoka Hospitali Laquintinie zilieleza kuwa, Koumate alifikishwa hospitalini hapo akiwa tayari ameshafariki dunia na ndiyo maana mkunga na wahudumu walipuuza kumpeleka wodi ya wazazi. Wahudumu walieleza kuwa mwili wa marehemu ulitakiwa kupelekwa mochwari lakini Agnes alisisitiza kuwa, mwili wa marehemu dada yake lazima ufanyiwe upasuaji ili kutoa wale watoto. 
Chanzo kiliendelea kueleza kuwa, Agnes alipuuzia ushauri wa wahudumu na kuamua kupasua tumbo la marehgemu dada yake chini ya veranda na kukuta watoto wote wawili wamefariki. Chanzo hicho kiliendelea kueleza kuwa, Koumate aliyekuwa akiishi Douala V, mwanzoni alimpelekwa na dada yake kwenye hospitali ya Wialaya ya Nylon huko Douala III na baadaye alipoona hali imebadilika alimhamishia Hospitali ya Laquintinie.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.