Stori: Mwandishi Wetu, Risasi
Kampala, Uganda: Kufuru ya
matumizi makubwa ya fedha inayofanywa na kijana mwenye uraia wa
Tanzania, Jack Pemba nchini Uganda, imewaacha midomo wazi mamia ya
wananchi wakati utajiri wake ukitikisa kila kona ya burudani.
Mapema mwaka jana, Jack Pemba alifanya
sherehe ‘bethidei’ ya kufuru wakati akisherekea kutimiza umri wa miaka
42, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Speke Resort Munyonyo iliyopo
pembezoni mwa Ziwa Victoria, nje ya Mji Mkuu wa Uganda, Kampala.
Kwa mujibu wa picha za mnato na video
zilizopatikana katika mitandao ambazo gazeti hili ‘linazishikilia’, Jack
Pemba anasikika akiyataja magari yake ya bei mbaya, yaliyoegeshwa
katika nyumba anayoishi, ambayo hata hivyo haijulikani kama ni Kampala
au Munyonyo. Anayataja aina ya magari hayo kuwa ni pamoja na 4 Matic,
Hammer H3, Aud, BMW X 6, Toyota Alphard na Range Rover Sport 2016.
Katika kile kinachoonekana kama
kulibariki gari lake jipya, Range Rover Sport 2016, katika video
nyingine, Jack Pemba anaonekana akiliosha na mvinyo aina ya Johnnie
Walker Black Label, unaotajwa kuwa ni miongoni mwa pombe zinazouzwa kwa
bei ghali.
ALETA NYODO KWENYE TUZO
Mei mwaka jana, Jack Pemba alialikwa
katika sherehe za utoaji tuzo zinazojulikana kama Abriyanz Fashion
Awards zilizofanyika kwenye Ukumbi wa MTN Arena, Lugogo, MC wa shughuli
hiyo, Roger Mugisha aliwatambulisha watu kuwa kulikuwa na mfanyabiashara
mkubwa kutoka Tanzania ambaye anaitwa Jack Pemba.
Alipomtaja jina na kumtaka kusimama ili
kuwapungia mikono waalikwa, Jack Pemba hakupunga, bali aliachia tabasamu
na kutoa burungutu la fedha na kuzirusha hewani noti za Uganda ambazo
zilianza kugombewa na watu wote waliokuwemo ukumbini. Inakadiriwa
alirusha kama milioni saba hivi kwenye tukio hilo.
WAGANDA WAHOJI, HUYU NI NANI?
Baadhi ya wadau wa burudani wa Uganda
wamekuwa wakihoji Jack Pemba anayeandikwa na vyombo vya habari nchini
humo ni nani, ingawa wanafahamu kuwa kijana huyo ni Mtanzania.
Wanashangazwa na mbwembwe zake kiasi kwamba anaonekana kuwafunika vijana
wanaounda kundi linalojulikana kama Rich Gang, ambalo linamhusisha pia
mume wa zamani wa mwandani wa Diamond Zarinah Hassan ‘Zari The Boss
Lady’, Ivan Semwanga.
Akiwa Uganda, Jack Pemba anatajwa kuwa
mtu anayependa sana kuvinjari na wasichana warembo na mara kadhaa, picha
zake zimeonekana akiwa na mabinti tofautitofauti.
Mtu mmoja aliyezungumza na gazeti hili,
aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwendapole, alisema anamfahamu Jack
kama kijana mpenda starehe na anayetaka uwepo wake kutambuliwa popote
anapokuwa.
Mmoja wa viongozi wa bendi ya FM
Academia, aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema staili ya maisha ya
kijana huyo siyo nzuri, kwani uzoefu wake unamuonyesha wengi huishia
pabaya.
“Jack Pemba ni mtu wetu, anawasaidia
sana wanamuziki wetu na kwa kweli sijui kwa sasa yupo wapi, wengine
wanasema yupo Sauz, wengine UK (Uingereza), lakini ninachokifahamu ni
kwamba starehe nyingi zinapofua.”
TUJIKUMBUSHE KUHUSU JACK PEMBA
Jack Pemba ni kijana wa Kitanzania
ambaye aliibuka na kupata umaarufu mkubwa mwishoni mwa miaka ya 2000,
baada ya kuwasili akitokea Uingereza, inakosemekana ana mke mzungu na
watoto.
Akiwa Bongo, Jack Pemba ambaye ni mkali
kwa ‘totoz’ alitembea na Aunt Ezekiel, lakini wakaachana miezi michache
baada ya kutoelewana.
Jack Pemba ni maarufu miongoni mwa
wanamuziki, kwani ni mmoja kati ya mapedeshee wanaofahamika kwa kutunza
kiasi kikubwa cha fedha jukwaani, huku akizawadiwa kwa kuimbwa kwenye
nyimbo.
CHEKI VIDEO YAKE HAPA

Note: Only a member of this blog may post a comment.