Msanii wa filamu Bongo, Glasnost Kalinga ‘Gilla’ katika pozi.
MSANII wa filamu anayekuja juu
Bongo, Glasnost Kalinga ‘Gilla’ kumbe ni mjasiriamali akiendesha
biashara ya Mamalishe maeneo ya Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
Kamera ya gazeti hili ilimnasa Gilla
akiwa bize katika mgahawa wake akihangaika huku na huko peke yake na
kusababisha watu wanaomfahamu kuwa na maswali vichwani mwao.
“Hii biashara nimeifungua muda siyo mrefu na kwa kawaida kuna wasichana wanaonisaidia lakini leo hawapo ndiyo maana nimekomaa mwenyewe ili hela isinipite.

Note: Only a member of this blog may post a comment.