Monday, February 29, 2016

Anonymous

Video ya MAN CITY Walivyoibuka Mabingwa wa Capital One Kwa Mikwaju ya Penati Dhidi ya LIVERPOOL

February 28 michezo migi ilipigwa Uingereza, lakini ukiachana na michezo ya Ligi Kuu Uingereza bado burudani kubwa ya soka ilikuwa ni katika mchezo wa fainali ya mechi ya Kombe la Ligi, fainali ambayo ilikuwa inazikutanisha Liverpool dhidi ya Man City.
Mechi hiyo ya Liverpool na Man City ilikuwa ngumu kupata mshindi kirahisi, kwani hadi dakika ya 90 zinamalizika, walikuwa wamefungana goli 1-1 goli la Liverpool lilifungwa na Philippe Coutinho dakika ya 83, baada ya Man City kupata goli la uongozi  dakika ya 49 kupitia kwa Fernandinho ,  hivyo ikalazimika wapigiane mikwaju ya penati.
31A752C200000578-3468255-image-a-75_1456684886110
Kwa upande wa mikwaju ya penati, bahati iliwaangukia Man City, kwani walifanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya penati 3-1,  LeivaCoutinho na Lallana ndio walikosa penati kwa upande wa Liverpool, huku upande wa Man City  Fernandinho ndio alikosa penati.
Video ya magoli ya Liverpool Vs Man City

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.