Wednesday, February 24, 2016

Anonymous

[VIDEO] MESSI 2 -ARSENAL 0: Lionel MESSI Msikie Tu... Avunja Rekodi Yake Hii Kwa PETR CECH

Usiku wa February 23 klabu ya FC Barcelona ya Hispania ilikuwa imesafiri kutoka Hispania hadi London Uingereza kukutana na Arsenal katika mchezo wao wa kwanza wa michuano ya klabu Bingwa barani Afrika, mchezo ambao ulikuwa wa hatua ya 16 bora, hivyo kila timu ilikuwa inahitaji ushindi.
317CE60D00000578-3460765-image-a-13_1456263390157
Mchezo ulimalizika kwa Lionel Messi kuipatia  FC Barcelona ushindi wa goli 2-0, magoli ya Lionel Messi yaliofungwa dakika ya 71 na 83, yalifanya mitaa mbalimbali ya London Uingereza kupooza, kwani ndio makazi ya mashabiki wengi wa Arsenal. 

Kwa matokeo hayo Arsenal italazimika kwenda Nou Camp kusaka ushindi wa zaidi ya goli mbili ili iweze kuiondoa FC Barcelona na wao watinge robo fainali. Hata hivyo ushindi wa goli mbili kwa Lionel Messi dhidi ya kipa wa Arsenal Petr Cech, unavunja mwiko wa Messi kutowahi kumfunga Petr Cech kwa jumla ya muda wa masaa 10 na dakika 11.
Kama hukupata nafasi ya kucheki mechi hii ndio video ya magoli ya Lionel Messi

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.