Monday, February 22, 2016

Anonymous

VIDEO: Kama Ulimiss Mechi ya CHELSEA Dhidi ya MAN CITY, Magoli Yote Yapo Hapa, Full Time 5-1 Feb 21


February 20 Kombe la FA Uingereza liliendelea kwa michezo mitatu kupigwa katika viwanja vitatu Uingereza, klabu ya Blackburn Rovers walikuwa wenyeji wa West Ham United, Tottenham Hotspur walikuwa wenyeji wa Crystal Palace, mwisho ukachezwa mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Man City.

Mchezo wa Chelsea dhidi ya Man City ndio mchezo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka, kwani ulikuwa unahusisha timu kubwa za Ligi Kuu Uingereza kwa siku ya February 21. Mchezo ulimalizika kwa Chelsea kuibuka na ushindi wa goli 5-1. Magoli ya Chelsea yalifungwa na Diego Costa dakika ya 35, Willian dakika ya 48, Gary Cahill dakika ya 53, Eden Hazard dakika ya 67 na goli la mwisho lilifungwa na Bertrand Traore dakika ya 89, wakati goli la kufutia machozi la Man City lilifungwa na David Faupala dakika ya 37.
 Tazama video hiyo hapa; 
Matokeo ya mechi nyingine za FA CUP
Tottenham Hotspur 0 – 1 Crystal Palace
Blackburn Rovers 1 – 5 West Ham United

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.