Friday, February 19, 2016

Anonymous

RAY KIGOSI: Nilishawahi Kumuokoa NAY wa Mitego Asipigwe na Kina WEMA SEPETU

STAA wa Bongo Movie, Vincent Kigosi ‘Ray’ kwa mara nyingine ameendelea kuteka ‘headlines’ baada ya kuibuka na kudai kuwa alishawahi kumuokoa staa wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego asipigwe.

Akizungumza asubuhi hii katika kipindi cha Leo Tena kinachorusha na Clouds FM, Ray alisema kuwa alipokuwa katika shoo ya Fiesta Mwanza, Nay alivamiwa na kundi la wasanii wa Bongo Movie na kutaka kupigwa.
 “Nilifanikiwa kumzuia kwa sababu wasanii walikuwa wengi wakiongozwa na Wema Sepetu sasa nashangaa mwenzangu Nay ananisakama natumia pesa zote za mauzo ya filamu namalizia kwenye mkorogo,” alisema Nay.
Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.