Wasanii hao wakihojiwa.
Stori: Gladness Mallya, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Kama hukuipata kwa kina
habari ya wasanii 22 wa kucheza ngoma za asili kutoka Sumbawanga na
Makambako, Risasi Jumamosi lina full stori ya wasanii hao ambao
wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kutapeliwa na kuletwa jijini Dar
kwa kile walichoambiwa kwamba wanasafirishwa kuelekea nchini Misri
kufanya shoo.
Chanzo
makini kilieleza kwamba, wasanii hao walisafirishwa hadi na Dar na
kutelekezwa katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Ponde iliyopo maeneo
ya Kigogo jijini Dar huku wakiwa na hali mbaya kwani walikuwa
wakibangaiza fedha ya kula kwa kukata mauno kwenye baa mbalimbali huku
wakisubiri mwenyeji wao awafanyie maandalizi ya kusafiri.
Baada
ya kupenyezewa habari hizo, paparazi wetu alifika katika nyumba hiyo ya
wageni ambapo watu hao walieleza kwamba waliletwa na mwenyeji wao
waliyemtaja kwa jina la Paulo Joseph Sinkala ambaye aliwaambia
anawapeleka Misri kwa ajili ya kucheza ngoma za asili.
“Yaani hapa tumewekwa kwenye vyumba
vitatu watu 22, tunalala kwa shida hata kula ni kwa shida ambapo imebidi
tuwe tunafanya shoo kwenye baa mbalimbali walau tupate fedha kwa ajili
ya kununua chakula,” walisema watu hao.
Barua walioiandika kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuomba msaada
Paulo alipoulizwa kuhusiana na suala
hilo alisema kwamba yeye ni mwenyekiti wa kikundi hicho na alikuwa
anafanya mpango wa kuwasafirisha wasanii wake hao kwenda kufanya shoo
nchini Misri pia alionyesha barua aliyoandika kwa niaba ya wenzake kwa
ajili ya kumfikia Rais John Magufuli.
Hata
hivyo, ilielezwa kuwa Paulo aliwachangisha wenzake hao kati ya sh
80,000 na 150, 000 kwa kuwarubuni kuwa kupitia kikundi chake cha
Wanyamwanga Simba Culture Group atawasafirisha kwenda kwenye tamasha la
sanaa kwa ufadhili wa rais Magufuli na mke wa rais mstaafu, Jakaya
Kikwete, Salma kitu ambacho hakikuwa na ukweli.
Paulo alishikiliwa na kituo cha polisi
cha Magomeni jijini Dar kwa ajili ya kujieleza zaidi huku watu hao
wakiwa wamebaki kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni wakiwa hawana la
kufanya.

Note: Only a member of this blog may post a comment.