Video Queen, Jack Cliff.
NA Imelda Mtema, Risasi JumamosiDAR ES SALAAM: Ikiwa imekatika miaka miwili tangu alipokamatwa na madawa ya kulevya huko Macau, nchini China, Video Queen, Jack Cliff ameibua simanzi upya baada ya kuandika barua ya wazi kwa Watanzania.
Simanzi hiyo iliibuka mwanzoni mwa wiki hii mara baada ya barua hiyo kusomwa redioni na Mtangazaji Millard Ayo ambapo barua hiyo ilieleza kuwa ameamua kufanya hivyo ili kuwaweka sawa wanaosambaza taarifa za uongo zinazomhusu.
…Akiwa katika pozi.
Katika barua hiyo, ameweka wazi kwamba anajuta kubeba madawa ya kulevya na mwisho wa siku kujikuta akiwa kwenye mikono ya polisi kitu ambacho hakukitegemea kabisa. Anahuzunika, ila pamoja na hayo yote, ameamua kuwaomba msamaha Watanzania wote kwa kile kilichotokea.“Inasikikitisha, Mungu amsaidie atoke jamani maana kama kujuta ameshajuta vya kutosha,” alisema John Jimy, mkazi wa Mwenge Dar.
Ingawa taarifa zinasema kwamba watu wengi wamekuwa wakienda gerezani nchini humo kumuona lakini mwenyewe amesema familia yake ndiyo pekee ambayo imekuwa ikimjali na kumtembelea mara kwa mara.

Note: Only a member of this blog may post a comment.