NA Mayasa Mariwata, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Tofauti na ilivyotarajiwa
na wengi, mastaa mbalimbali Bongo wameukacha msiba wa mkongwe wa Bongo
Fleva, Michael Dennis ‘John Woka’ aliyefariki dunia Jumanne iliyopita
baada ya kulipukiwa na mtungi wa gesi ya gari iliyokuwa kwenye
matengenezo.
Kitendo cha mastaa kutoonekana msibani
kilijidhihirisha Jumatano iliyopita kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili
jijini Dar, wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Woka uliosafirishwa
kwenda jijini Tanga kwa ajili ya mazishi yaliyotarajiwa kufanyika katika
Makaburi ya Sahare jijini humo.
“Mmh! Hawa wasanii wa Bongo wana roho
mbaya kwa kweli mbona leo hawapo hapa sitaki kuamini kama kuna mtu
hamjui John Woka, hapa namuona H. Baba (Hamis Ramadhan), Sajenti (Husna
Idd), Stara Thomas, Keisha (Khadija Shabani) na Ado Novemba wengine wote
wameingia mitini kweli?” alihoji mmoja wa wafiwa.
Baada ya kusikia dukuduku hilo, paparazi wetu alizungumza na H. Baba ambaye asema amechukizwa na kitendo cha mastaa wa muziki kutojitokeza msibani hapo na kusema kuwa, wengi wao wanapenda mauzo huenda walihisi siku hiyo hawatauza sura.
Msanii
mkongwe wa bongo fleva, Mgosi Mkoloni (mwenye fulana nyekundu) akiaga
pamoja na waombolezaji wengine katika kuuaga mwili wa marehemu.
“Walichokifanya siyo sawa kabisa wengine
kazi yao ‘kupost’ mitandaoni msibani hawaji, lazima wakumbuke mauzo
yote ya hapa duniani mwisho wa siku lazima kila mmoja arudi kwenye
udongo, isitoshe jana haikuwa wikiendi kusema wamechoka na wala kipindi
hiki hakuna shoo,” alisema H. Baba.
Naye msanii wa filamu Bongo, Husna Idd ‘Sajent’ alisema wasanii wengi walikuwa na taarifa, licha ya kusikia kwenye vyombo vya habari taarifa zilitumwa kwenye makundi yote ya wasanii.
Naye msanii wa filamu Bongo, Husna Idd ‘Sajent’ alisema wasanii wengi walikuwa na taarifa, licha ya kusikia kwenye vyombo vya habari taarifa zilitumwa kwenye makundi yote ya wasanii.
“Huu msiba umeniuma kweli, jamaa alikuwa
mtu wangu wa karibu sana na hata kipindi cha nyuma niliwahi kuuza sura
kwenye wimbo wake, nimeumia wasanii wenzangu kutofika katika msiba wake,
kifupi hatuna umoja na tuna ubaguzi,” alisema ‘Sajent.’
Msanii wa bongo fleva, Hamis Ramadhan, “H-Baba”

Note: Only a member of this blog may post a comment.