Video Queen anayeshaini kwenye tasnia ya Bongo Movie, Gift Stanford ‘Gigy mone’.
Na Nyemo Chilongani, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Video
Queen anayeuza nyago kwenye video mbalimbali Bongo, Gift Stanford ‘Gigy
Money’ yamemkuta mazito kwa kutupiwa matusi mazito baada ya kuweka picha
inayomuonesha akiwa amevaa kihasara katika Mtandao wa Kijamii wa
Instagram.
Tukio
hilo lilitokea juzikati ambapo msanii huyo ambaye amekuwa na desturi ya
kutupia picha za nusu utupu mtandaoni, kutupia moja aliyoonekana anavua
suruali na kubaki na kibukta kifupi.
Baada ya kutupia picha hiyo,
kilichofuata kutoka kwa wafuasi wa mtandao huo ni kumvurumishia matusi
mazito ambayo hayaandikiki gazetini huku wengine wakienda mbali kwa
kusema atakuwa amelaaniwa.
“Huyu si bure, atakuwa amelaaniwa.
Huwezi kuweka picha kama hizi kwenye mitandao ya kijamii kama una malezi
mazuri ya wazazi. Ni laana hii inayomsumbua,” aliandika mdau mmoja
mtandaoni huku mwenzake akiunga mkono:
“Huyu
dada anajiaibisha sana, hii picha si ya kuweka hadharani namna hii,
sasa angalia anavyoambulia matusi. Mimi namuonya tu awe makini kwani
bado kuna sheria kali za mitandaoni.”

Mara baada ya kushuhudia matusi hayo
mtandaoni, gazeti hili lilimtafuta Gigy kwa njia ya simu ambaye
alionekana kutoshangazwa na matusi hayo.
“Nawashangaa sana wote wanaonisema kisa picha, mbona ya kawaida sana, yaani kama mtu anashangaa picha kama hiyo, za kina Nick Minaj atasemaje? Kwangu naona picha za kawaida kwani nimevaa nguo ambazo natembea nazo barabarani,” alisema Gigy.
“Nawashangaa sana wote wanaonisema kisa picha, mbona ya kawaida sana, yaani kama mtu anashangaa picha kama hiyo, za kina Nick Minaj atasemaje? Kwangu naona picha za kawaida kwani nimevaa nguo ambazo natembea nazo barabarani,” alisema Gigy.
Note: Only a member of this blog may post a comment.