Friday, February 19, 2016

Anonymous

Kama JOSE MORINHO akitua MAN United, Hawa Ndio Mastaa wa Soka Watakaojiunga Naye


Baada ya uvumi wa muda mrefu sasa kila shabiki wa soka la Uingereza hususani wa klabu ya Man United anatamani msimu umalizike ili zile stori zinazoandikwa sana na kuongelewa katika vyombo vya habari zipatiwe majibu yake. Kwa zaidi ya wiki tano sasa klabu ya Man United inahusishwa kutaka kumtimua kazi kocha wake Louis van Gaal na kumpa nafasi hiyo Jose Mourinho.

Bado stori za Mourinho kujiunga na Man United zinazidi kuandikwa na kuzungumzwa kila kukicha, ila Mourinho anahusishwa kuwa atajiunga na Man United baada ya msimu wa Ligi Kuu Uingereza kumalizika, kitu ambacho kinafanya mashabiki wa soka wawe na shauku ya kutamani Ligi iishe ili mwisho wa msimu wajue stori hizo ni kweli au tetesi?

Zlatan
February 18 101greatgoals.com wameandika stori za Jose Mourinho kuwa na mipango ya kuwasajili mastaa hawa ili waungane nae ndani ya klabu ya Man United mwishoni mwa msimu wa 2015/2016.
Majina yanayotajwa kufuatiliwa na Jose Mourinho ni pamoja na kiungo wa AS Roma Radja Nainggolan na mshambuliaji wa Sweden na klabu ya PSG Zlatan Ibrahimovic. Hivyo bado tetesi za ukweli wa Mourinho kujiunga na Man United zitajulikana mwisho wa msimu.

Radja Nainggolan

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.