Headlines za kocha wa zamani wa vilabu vya Real Madrid na Chelsea ya Uingereza Jose Mourinho February 23 ameingia kwenye headlines baada ya kuonesha viashiria vingine vya kuwa anakaribia kuhamia jiji la Manchester ambalo ndio makao makuu ya klabu ya Man United yalipo.
Jose Mourinho tayari anatajwa kutafuta na kupata nyumba ya kuishi katika jiji la Manchester na baadhi ya magazeti mengine yameandika kuwa tayari kapata nyumba na yupo katika mchakato wa kununua vitu vya ndani. Klabu ya Man United ambayo ipo nafasi ya 5 katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza kwa kuwa na point 41 .
Gazeti la Ureno Correio da Manha ni moja kati ya magazeti yalioandika stori hii.

Note: Only a member of this blog may post a comment.