Katika mwezi huo uliokuwa na raundi tatu, Kapombe alicheza dakika zote 180 za mechi mbili za timu yake dhidi ya African Sports na Mgambo Shooting. Mechi ya tatu ya Azam FC katika raundi hiyo dhidi ya Tanzania Prisons ilikuwa kiporo na ilichezwa Februari 24, 2016.
Taarifa iliyotumwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jana ilisema Kapombe amefanikiwa kuchukua tuzo hiyo baada ya kufunga mabao yote mawili kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mgambo Shooting. Pia alisaidia kupatikana bao la Azam kwenye mechi dhidi ya African Sports iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Kufuatia kupata tuzo hiyo, Kapombe atazawadiwa kitita cha Sh 1,000,000 na wadhamini, Vodacom.

Note: Only a member of this blog may post a comment.