Wachezaji wa Yanga wakishangilia kwa pamoja.
SIMBA haitaki mchezo kwani kesho Jumapili itashusha kikosi kamili
kupambana na Singida United katika mchezo wa Kombe la FA kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba itaingia uwanjani na kumbukumbu ya kufungwa mabao 2-0 na Yanga wikiendi iliyopita kwenye uwanja huo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Simba itaingia uwanjani na kumbukumbu ya kufungwa mabao 2-0 na Yanga wikiendi iliyopita kwenye uwanja huo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Kocha wa Simba, Jackson Mayanja, ameliambia Championi Jumamosi kuwa
katika mechi hiyo hatafanya masihara na atahakikisha anatumia silaha
zake zote ili kupata ushindi.
“Sitaki aibu kwani wapinzani wetu ndiyo kwanza wamepanda daraja kutoka
daraja la pili hadi la kwanza, tukifanya mchezo wanaweza kutufunga,
sitaki itokee hali hiyo.
“Tumejipanga kuhakikisha tunashinda mechi hiyo na hatutaki masihara kabisa kwa sababu Kombe la FA lina umuhimu mkubwa sana kwetu kwani tunataka kucheza michuano ya kimataifa,” alisema Mayanja.
“Tumejipanga kuhakikisha tunashinda mechi hiyo na hatutaki masihara kabisa kwa sababu Kombe la FA lina umuhimu mkubwa sana kwetu kwani tunataka kucheza michuano ya kimataifa,” alisema Mayanja.
Kwa upande wake Kocha wa Singida United, Frugence Novatus, alisema:
“Mechi hiyo ni ngumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo
mazuri ambayo yatatuwezesha kusonga mbele.”
Mechi nyingine za Kombe la FA kesho ni kati ya Panone ya Kilimanjaro na Azam FC ya Dar kwenye Uwanja wa Ushirika Moshi wakati Toto Africans itacheza na Geita Gold kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Note: Only a member of this blog may post a comment.