Beki tegemeo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Suleiman Hassan, PembaLICHA ya Kocha wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm kujaribu kumshawishi nahodha wake na beki tegemeo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kufanya mazoezi, mchakato huo umeonekana kuwa mgumu na kuna uwezekano Cannavaro akakosa mechi ya kesho Jumamosi dhidi ya Simba.
Cannavaro aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu, alirejea uwanjani hivi karibuni lakini hajacheza mechi hata moja, alifanya mazoezi na wenzake kwa siku kadhaa lakini juzi hali ilibadilika na kushindwa kujumuika na wenzake katika mazoezi kwenye Uwanja wa Gombani.
Pamoja na hivyo, hakuna kiongozi wala mtu yeyote wa benchi la ufundi aliyekuwa tayari kuzungumzia afya ya mchezaji huyo. Yanga imekuwepo Pemba kwa kambi ya wiki moja ikijiandaa kuivaa Simba katika Ligi Kuu Bara, kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini

Note: Only a member of this blog may post a comment.