Jana December 07 2015 kamati kuu ya Chama cha CCM ilifanya kikao kikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.
Leo Katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amefanya mkutano leo kuzungumzia yale ambayo yamezungumzwa ndani ya kikao hicho cha jana.
Pongezi kwa Serikali ya Rais Magufuli >>>> “Kama
Chama tunaunga mkono juhudi zao na tunaahidi kuwaunga mkono.. Kamati
kuu inaunga mkono juhudi za Rais wa sasa kuhusu mamlaka za mapato
kusimamiwa ipasavyo, juhudi hizi za awamu ya tano kwa muda mfupi zimezaa
matunda yanayoonekana, kamati inawataka wahusika wote watoe ushirikiano
kwa wahusika wote“- Katibu Mkuu CCM, Abdulrahman Kinana

Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana akimpigia salute Rais Magufuli.
Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana akimpigia salute Rais Magufuli.
“Kamati
kuu kama ilivyoagizwa na ilani ya uchaguzi, tumefurahi kuona
wanasimamia matumizi yasiyo ya lazima kwa Serikali, lazima tumuunge
mkono.. pia tunawataka wanaCCM na wananchi wote kumuunga mkono Rais kwa
kufanya kazi kwa maarifa na uadilifu, kujituma ili kujenga nchi yetu“- Abdulrahman Kinana

Rais Magufuli, Waziri Mkuu Majaliwa na Makamu wa Rais Mama Samia.
Rais Magufuli, Waziri Mkuu Majaliwa na Makamu wa Rais Mama Samia.
Hayo ni machache kutoka kwenye Kikao cha CCM walivyojadili Serikali ya Rais Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu pamoja na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim kwenye kasi yao.

Note: Only a member of this blog may post a comment.