Headlines za David Kafulila wa Chama cha NCCR–
Mageuzi kuamua kufika Mahakama kuu ya Tabora kuhusu sababu ya matokeo
ya Uchaguzi Mkuu kuonesha hakupata Kura za kutosha ili awakilishe
wananchi wa Kigoma Kusini.
Sasa kilichoendelea ni kwamba Mahakama
Kuu kanda ya Tabora imemua Kafulila kulipa Milioni 7.5 badala ya Milioni
15 kama dhamana ya kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi katika jimbo la
Kigoma Kusini iliyofunguliwa na David Kafulila dhidi ya washtakiwa Husna Mwilima,Mkurungezi wa Halmashauri ya wilaya ya Uvinza, msimamzi wa Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
‘Leo mahakama
kuu ya Tabora shauri langu la ombi la kukadiria la kugharamia kama
dhamana ya kesi lilisikilizwa kwa mara ya mwisho, kwa sababu lilianza
kusikilizwa jana na leo jaji aliweza kuamua baada ya kuzingatia pande
zote mbili na kusema nilipe kiasi cha Milioni 7.5 badala ya shilingi
milioni 15 ambayo ilikuwa imepangwa na mwanasheria wa Serikali pamoja na
wakili wa Husna Mwilima’ -David Kafulila
‘Katika
kesi hii washtakiwa ni Husna Mwilima pamoja na msimamizi wa Uchaguzi kwa
hiyo katika utaratibu wa kawaida kwamba mtu anapofunguka kesi ya
Uchaguzi anatakiwa alipe dhamana isiyozidi milioni 5 kwa kila
anayemshtaki…. kwahiyo katika hali kawaida maana yake ningelipa milioni
15 lakini kwa mujibu wa sheria ni uamuzi wa jaji kuamua kama
anayeshtakia alipe kiasi gani au anaweza asilipe kiasi chochote‘>>> – David Kafulila
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza David Kafulila
Note: Only a member of this blog may post a comment.