Polisi akiupiga picha mwili wa marehemu.
SIMANZI! Ramadhan Mohamed Duku
(52), mkazi wa Mji Mpya mjini hapa amekutwa akiwa amekufa kwenye nyumba
ya kulala wageni (gesti) aliyokuwa akiilinda hivyo kuibua taharuki kubwa
kwa wateja waliolazimika kutoka nduki na kuwaacha michepuko waliokuwa
nao vyumbani.
Tukio hilo lililoibua utata juu ya kifo hicho, lilijiri wiki
iliyopita katika Gesti ya Uswaa iliyopo maeneo hayo ya Mji Mpya ambapo
mwanaume huyo huwa ni mlinzi wa kujitegemea aliyekuwa akilinda gesti
mbili tofauti.
Wafiwa wakilia kwa huzuni kubwa.
Ilielezwa kwamba, mchana alikuwa akilinda gesti iitwayo Simtu Baba
iliyopo Stendi ya Daladala ya Mji Mpya na usiku alikuwa akilinda Gesti
ya Uswaa iliyopo maeneo hayohayo jirani na soko ambako ndiko alikokutwa
na umauti.
Akiwa kwenye misele ya kutimiza majukumu yake ya kikazi, majira ya
saa 2:00 usiku, mwanahabari wetu alifika kwenye gesti upande wa baa na
kuzungumza na jamaa huyo aliyeonekana kuwa na afya njema akifuatilia
taarifa ya habari ya runingani kuhusu Rais John Pombe Magufuli
anavyowanyoosha watumishi wabovu serikalini.
Katika hali ya mshangao, asubuhi yake, mwandishi wetu alipigwa na
butwaa alipopigiwa simu na mmoja wa wahudumu wa gesti hiyo akimjulisha
kutokea kwa kifo hicho.
Mwili wa marehemu ukitolewa ndani ya gest hiyo.
Mwandishi wetu alifika eneo la tukio na kushuhudia umati ukiwa nje ya
gesti hiyo huku geti likiwa limefungwa na funguo alikuwa nazo marehemu
hivyo wageni kushindwa kutoka na wengine kuruka ukuta wakidaiwa
kuikimbia michepuko yao na kuogopa kutoa ushirikiano kwa polisi.
Muda mfupi baadaye, polisi walifika eneo la tukio na kuruka ukuta
kisha kumkagua marehemu ambapo walifanikiwa kumkuta na funguo mfukoni
ndipo wakafungua geti na kuwataka wateja wote waliokuwa ndani ya gesti
hiyo kwenda kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo huku ndugu wa marehemu
waliofika eneo hilo wakiangua vilio na kugaragara chini.
Watu wakiwa nje ya gesti alimofia.
Baadaye polisi waliwaachia wateja hao ambapo waliuchukua mwili wa
marehemu na kwenda kuuhifadhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Morogoro huku uchunguzi wa kifo hicho cha ghafla ukiendelea kubaini
chanzo chake.
Akizungumza na gazeti hili, mmiliki wa gesti hiyo, Alnod Ndossi
alithibitisha mlinzi wake kufa ghafla akiwa kazini huku akiacha mke na
watoto watatu.
Mmoja wa wateja waliokuwa kwenye gesti hiyo waliozungumza na mwandishi wetu juu ya tukio hilo, Ally Shomari alikuwa na haya ya kusema:
Mmoja wa wateja waliokuwa kwenye gesti hiyo waliozungumza na mwandishi wetu juu ya tukio hilo, Ally Shomari alikuwa na haya ya kusema:
Mwili wa marehemu ukipakizwa kwenye gari.
“Nilipofika kwenye gesti hii majira ya saa 4:00 usiku nilimkuta jamaa
akiendelea na majukumu yake ndipo nikaingia kulala. Nilishtuka kusikia
watu wakiruka ukuta na nilipotoka nikakuta jamaa amekata roho akiwa
amekaa kwenye kiti pembeni mwa mlango wa vyumbani.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.